Nenda kwa yaliyomo

Kisiwa cha Mombasa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchwa katika kahawia, iliyopatikana kwenye Kisiwa cha Mombasa, kikiwa maonyeshoni katika Houston Makumbusho ya Sayansi ya Asili.

Kisiwa cha Mombasa kinapatikana kwenye bahari ya Hindi karibu sana na pwani ya nchi ya Kenya na kinaunganishwa na bara kupitia "Makupa Causeway" upande wa Magharibi, daraja la Nyali upande wa Kaskazini na kivuko cha Likoni upande wa Kusini.

Jiji la Mombasa linapatikana kisiwani.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mji wa kale wa Mombasa upo upande wa Mashariki mwa ufuo wa kisiwa hicho. Kilindini na Port Reitz ndiyo bandari za kisasa zenye vina virefu na zinatenganisha kisiwa na bara la Kenya kwa upande wa kusini.

Bandari ya kale inayojulikana kama Tudor na ilitumika kulinda Fort Jesus na Tudor Creek zinatenganisha kisiwa na bara upande wa Kaskazini. Maeneo ya kisasa ya makazi na maeneo ya viwanda yanapatikana kwenye sehemu nyingine za kisiwa.

Bandari ya Tudor na Tudor Creek zilipata majina yake kutoka kwa nahodha Owen Tudor wa Royal Navy ambaye alikuwa wa kwanza kutafiti eneo hilo.

Kisiwa cha Mombasa ni moja kati ya tarafa nne za Kaunti ya Mombasa na kinagawanywa katika migawanyiko sita[1]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-18. Iliwekwa mnamo 2016-05-16.